Sabby: Ndoa Ilinipotezea Muda

IJUMAA WIKIENDA | Over Ze Weekend

DUH! Kwa mara ya kwanza tangu ndoa yake ivunjike mwaka jana, msanii wa filamu na Bongo Fleva, Sabrina Omary ‘Sabby’ ameweka wazi kuwepo ndani ya ndoa kulimpotezea muda mwingi kwani angekuwa amefika mbali.

Sabby Angel katika pozi

Akizungumza na Over Ze Weekend akiwa lokesheni kwenye maandalizi ya tamthiliya mpya, Sabby anayebamba pia na Ngoma ya Inahusu alisema kwa sasa muziki ndiyo kila kitu kwake na suala la ndoa amelipa kisogo.

“Nimedhamiria kweli na kama inavyoonekana natrend sana na Wimbo wa Inahusu. Ukija kwenye tamthiliya hapa tunaandaa mpya jina lake litajulikana baadaye lakini pia zipo zinazoendelea kuoneshwa. Sipendi na sitaki tena kurudi nyuma. Ujue nini? Ndoa ilinipotezea muda mwingi yaani hapa nisingeolewa ningekuwa nimefika mbali sana,” alisema Sabby.

Sabby aliolewa mwaka jana na Mwarabu aliyefahamika kwa jina la Jaruf lakini ndoa hiyo haikudumu.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Save

Save

Save

Save

Save

Save


Loading...

Toa comment