The House of Favourite Newspapers

Sabby: Zari hanifikii kwa lolote

0

sabby-2Sabby Angel

Stori: Hamida Hassan, Wikienda

DAR ES SALAAM: STAA wa sinema za Kibongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ameibuka na kusema kuwa anawashangaa wanaodai kuwa, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ni mwanamke mrembo wakimlinganisha na Wema Isaac Sepetu wakati kwake yeye hata hamfikii kwa lolote na anaamini kuwa wanawake wa Kitanzania ni warembo zaidi kuliko wa nchi nyingine.

zariZari The Boss Lady

Akichonga na mtandao wa Global Publishers, Sabby alisema kuwa yeye anachoona kwa Zari ambaye ni mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni kuwa na bahati tu ya kuwa na baba Tiffah lakini haoni uzuri alionao kwa sababu hata akipambanishwa naye atamfunika kwa uzuri.

“Nina mguu na shepu inayoendana na mwili wangu, huwezi kunilinganisha na Zari, najiamini na kama kuna mtu ana uwezo wa kufanya mashindano hayo afanye aone,” alisema Sabby.

Sabby aliamua kufunguka hayo kwa sababu kila akiingia mtandaoni anaona watu wakimzungumzia Zari kuwa ni mrembo na kusahau kuwa kuna wanawake wa Kibongo ambao ni warembo zaidi yake.

Leave A Reply