Sabrina: Sportpesa Tumejitahidi Kukabiliana na Changamoto Mbalimbali

Sabrina Msuya Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Sportpesa

SABRINA Msuya Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Sportpesa ametembelea studio zetu za Global Radio na Global TV na amebainisha kuwa licha ya mafanikio iliyoyapata Sportpesa lakini kuna baadhi ya changamoto imepitia na kukabiliana nazo katika kipindi cha miaka 5 tangu kutambulishwa kwake nchini Tanzania.

 

Sabrina amesema moja ya mafanikio ambayo Kampuni hiyo inajivunia ni kusaidia kukuza mpira wa miguu nchiniTanzania kupitia udhamini wake kwa baadhi ya vilabu vya Simba, Yanga na Namungo.

Sabrina Msuya Meneja Mahusiano wa SportPesa akiwa ndani ya Studio za Global TV na 255globalradio

Amebainisha kuwa, Licha ya kwamba SportPesa ndiyo mdhamini mkubwa wa Klabu ya Simba na jina lake la udhamini linakaa mbele ya jezi ya Simba lakini lilipofika suala la Simba kuvaa jezi zake bila logo ya udhamini wa Kampuni hiyo katika michezo yake ya Kimataifa, SportPesa iliamua ni vema kukubaliana kuweka Tangazo la Visit Tanzania ili kuitangaza Tanzania kimataifa.

 706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment