The House of Favourite Newspapers

SADC Yaidhinisha Brigedia Jenerali Nkangaa Kuwa Mkurugenzi wa Asasi ya Siasa

0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (katikati) pamoja na viongozi wengine

 

Baraza la mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) limeidhinisha jina la Mtanzania,Brigedia Jenerali Juma Nkangaa Sipe kuwa Mkurugenzi wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama katika sekretarieti ya SADC.

 

Akizungumzia hatua hiyo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema suala la ulinzi na usalama katika Bara la Afrika ni mojawapo ya viapumbele vya Tanzania ili kutoa fursa ya ufanywaji wa biasahara kutokana na uwepo wa amani na hivyo kuiwezesha Afrika kupiga hatua za kimaendeleo sawa na mabara mengine duniani

 

Waziri wa Mambo ya Nje Brigedia Jenerali Juma Nkangaa Sipe anachukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Mkurugenzi asasi hiyo Bw Jorge Kodoso kutoka Jamhuri ya Angola kumaliza kipindi chake cha miaka nane.

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya mchakato wa Kiswahili kutumika kisheria katika vikao vya SADC Mkurugenzi wa Jumuiya za Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agness Kayola amesema Tanzania imewasilisha pendekezo la la kufanyiwa marekebisho kwa Mkabata wa uanzishwaji wa SADC ili kukitambua Kiswahili kisheria kama mojawapo ya lugha nne rasmi katika shughuli za SADC

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa kawaida wa 42 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unatarajiwa kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye atawasili Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumanne ya Agosti 16,2022

Leave A Reply