The House of Favourite Newspapers

Safaree Akiri Kusalitiwa na Nicki Minaj Kisa Meek Mill

 

Nick Minaj na Mick Meel (Kushoto) na Kulia ni Safaree

ALIYEKUWA mpenzi wa Mwanamuziki wa Hip Hop, Nicki Minaj, Safaree Samuels amefanya mahojiano na kipindi cha mtangazaji Wendy na kukiri kuwa Nicki alimsaliti na kumpa penzi Meek Mill kitendo ambacho kinamuumiza mpaka leo.

Safaree alimwaga machozi alipokuwa akiongelea tukio hilo ambapo alisema kuwa, Nicki alimsaliti na kuanzisha uhusiano na rapa Meek tena kipindi hicho wakiandaa albamu ya pamoja lakini alihakikisha jamaa huyo naye anasalitiwa na kuendeleza penzi na Nicki kimyakimya siri ambayo hakuwahi kuiweka wazi.

“Mwaka uliopita tulikuwa pamoja, tuliongelea tofauti zetu lakini hata hivyo moja kwa moja Nicki ndiyo mwenye shida zaidi,” alisema Safaree.

Nick Minaj

Nicki kwa sasa anabanjuka na rapa Future ambapo uhusiano wao waliuanzisha wakiwa studio katika kutengeneza wimbo mpya na hii huenda ndiyo sababu ya Safaree kuamua kufunguka hadharani kwa kuwa bado anampenda japo Future anafanya juu chini kumhamisha bibi’ye huyo mji ili kumsahaulisha machungu ya mapenzi.

 

Comments are closed.