The House of Favourite Newspapers

Safari 1,054 Za Futwa Kisa Mgomo Ujerumani

Ground services employees from the Verdi union protest during strike action at Munich International Airport in Munich, Germany, on Friday, Feb. 17, 2023. Germany’s two largest airports, Frankfurt and Munich, came to a virtual standstill today as ground staff stage another strike over pay, exacerbating an already chaotic week for air travel after a system outage brought down Deutsche Lufthansa AGs operations two days ago. Photographer: Michaela Rehle/Bloomberg

Mgomo mkubwa wa wafanyakazi wa viwanja vya ndege nchini Ujerumani umeendelea, ukisababisha kufutwa kwa maelfu ya safari za ndege za ndani na kimataifa. Viwanja 13, vikiwemo vikubwa vya Munich na Frankfurt, vimeathirika baada ya mgomo wa saa 24 kuanza saa 6:00 usiku wa kuamkia Jumatatu, Machi 10.

Wanaogoma ni wafanyakazi wa sekta ya umma ndani ya viwanja vya ndege, maafisa wa maeneo ya kuruka na kutua ndege, pamoja na maafisa wa usalama wa viwanja hivyo. Katika uwanja wa ndege wa Frankfurt, safari 1,054 kati ya 1,116 zilizopangwa kwa siku hiyo zilifutwa, kwa mujibu wa shirika la habari la Ujerumani, dpa.

Kwa ujumla, mgomo huo unatarajiwa kufuta safari zaidi ya 3,400, ukiathiri takriban abiria 510,000 kote nchini. Viwanja vya ndege vya Berlin, Hamburg, Cologne/Bonn, na Munich vimesitisha safari nyingi, huku abiria wakishauriwa kutegemea ratiba zenye ndege chache sana.

Muungano wa vyama vya wafanyakazi wa Verdi ulisema mgomo huo umeathiri viwanja vikubwa vya Hamburg, Bremen, Hannover, Berlin, Duesseldorf, Dortmund, Cologne/Bonn, Leipzig/Halle, Stuttgart, na Munich. Katika viwanja vidogo vya Karlsruhe/Baden-Baden na Weeze, ni maafisa wa usalama pekee waliogoma.

Mgomo huu, unaojulikana kama “mgomo wa onyo,” ni mbinu ya kawaida katika majadiliano ya mishahara nchini Ujerumani. Umechochewa na mizozo miwili: moja ikiwa ni madai ya malipo na masharti bora kwa maafisa wa usalama wa viwanja vya ndege, na nyingine ikiwa ni mgogoro mpana wa mishahara kwa wafanyakazi wa serikali za majimbo na serikali kuu.

Mazungumzo kuhusu mgogoro wa mishahara yanatarajiwa kuanza tena Ijumaa, huku duru nyingine kwa maafisa wa usalama wa viwanja vya ndege ikipangwa kufanyika Machi 26 na 27.