Safari ya Kwenda Kutibiwa India, Hawa Nitarejea Akwama Airport

MSANII wa Bongo Fleva Hawa wa Nitarejea, amejikuta akirudishwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) baada ya kutotimiza vibali vya kusafiri vya kimatibabu kwenda India.

Meneja wa Msanii Diamond Platinumz, Babu Tale amesema hali hiyo imewakuta wakiwa tayari wameingia ndani ya uwanja wa ndege na kuanza kukaguliwa nyaraka zao mbalimbali na kwamba nyaraka iliyowakwamisha kusafiri ni kibali cha daktari kuelezea hali ya mgonjwa ili wahudumu ndani ya ndege wajue namna watakavyomhudumia.

 

“Mgonjwa anaweza akazimia au kutapika, anatakiwa ahudumiwe tofauti, imeshindikana kwa kuwa hakuna hizo nyaraka inayoonyesha hivyo kutoka kwa daktari na tumeambiwa turudi zitakapokamilika,” alisema Tale.

Hawa, Babu Tale na mama yake, Ndagina Hassan ilikuwa waondoke juzi Oktoba 13, 2018 saa 10:45 na ndege ya Shirika la Emirates ambapo Hawa na mama yake walifika uwanjani hapo tangu saa 7:00 mchana huku Babu Tale akiwasili saa 9:00 alasiri. Hawa amewaomba Watanzania kumuombea dua katika matibabu yake.

EXCLUSIVE Alikiba: “Kutekwa kwa MO Dewji Nimeguswa Sana”

Loading...

Toa comment