The House of Favourite Newspapers

Safari ya Tambwe Burundi, Yanga yapata kiwewe

0

AmissTambwe2

Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe.

Na Wilbert Molandi
WAKATI wenzake wakijiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC, mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, atakosa maandalizi hayo kutokana na kubanwa na majukumu ya timu yake ya taifa.

Yanga imeingia kambini juzi Jumatatu kwenye Hoteli ya Landmark, Kunduchi jijini Dar es Salaam ikijifua kwenye Uwanja wa Boko Veterani.

Mrundi huyo aliondoka nchini hivi karibuni kwa ajili ya kwenda kuichezea timu ya taifa katika mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia mchezo unaopigwa leo.

Akizungumza na Championi Jumatano, kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, alisema kuwa wachezaji wote walitarajiwa kuripoti kambini jana Jumanne kasoro Tambwe pekee anayemalizia majukumu yake ya timu ya taifa.

Pluijm alisema Mrundi huyo anatarajiwa kutua nchini leo Jumatano usiku mara baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa na kesho Alhamisi asubuhi atajiunga na wenzake kambini kujiandaa na mechi ya Azam.

“Wachezaji wote wanatarajiwa kuripoti kambini kesho (jana), waliokuwepo kwenye majukumu ya timu zao za taifa, isipokuwa Tambwe mwenyewe yeye ataripoti kambini keshokutwa (Alhamisi).

“Tambwe atachelewa kujiunga kwenye kambi ya pamoja ya kujiandaa na mechi na Azam kutokana na timu yake ya taifa kucheza mechi kesho (leo), hivyo mara baada ya mechi usiku atarejea nchini na moja kwa moja ataingia kambini.

“Wakati Tambwe akiwa kwenye majukumu hayo ya timu ya taifa, mimi ninaendelea na programu nyingine za kukiandaa kikosi changu kwa kuziboresha sehemu zenye upungufu,” alisema Pluijm.

Hata hivyo, hali hiyo imekuwa ikiwapa hofu mashabiki na baadhi ya viongozi wa timu hiyo kwa kuwa wengine wanaamini kuwa anaweza kupata majeraha kwenye mchezo wa leo na kushindwa kucheza mchezo a Jumamosi dhidi ya Azam, huku Wengine wakiamini kuwa uchovu unaweza kumzuia kuwa na kasi ileile ya mwanzo.

Leave A Reply