Safirisha Mizigo Yako Kirahisi kwa GNM Cargo

KAMA wewe ni mfanyabiashara mkubwa au mdogo, bila shaka ndoto zako ni kwenda kuagiza mzigo nje ya nchi, hususan nchini China ambako bidhaa nyingi hupatikana kwa bei nafuu lakini kinachowatatiza wengi, ni kwamba hawajui wapi pa kuanzia.

 

Habari njema ni kwamba, Kampuni ya GNM Cargo ambayo imebobea kwenye shughuli za usa_irishaji mizigo kutoka nchini China kuja Tanzania na nchi za Afrika Mashariki, ikiwa na uzoefu wa miaka kumi, sasa inakurahisishia mfanyabiashara katika safari zako za kufuata mzigo nchini China, kwa bei nafuu kabisa.

 

Uzuri ni kwamba, huhitaji kuwa na mtaji wa mamilioni ya fedha kufuata mzigo China, hata wafanyabiashara wadogo wanaweza kumudu kwani kampuni ya GNM, inatoza kiwango kidogo cha fedha ambacho mfanyabiashara yeyote anaweza kumudu.

 

Jinsi kampuni hiyo inavyofanya kazi, ni kwamba inamsaidia mfanyabiashara kwanza kwa maandalizi ya safari kutoka Tanzania kwenda nchini China. Hata kama hujawahi kufika China na huna mwenyeji, huna haja ya kuwa na hofu, GNM watakusimamia kwa kila kitu.

 

Kwanza watakusaidia kukutumia barua ya mualiko (Invitation letter) kutoka China ambayo utaitumia kwenye mchakato wa kuandaa safari, ikiwa ni pamoja na kupata Visa ya kuingia nchini humo. Kama hiyo haitoshi, mara baada ya kuwasili nchini China tu, utapokelewa na wenyeji wako kuanzia uwanja wa ndege na watakupeleka mpaka kwenye hoteli utakayofikia bure kabisa!

 

Baada ya kufika hotelini na kupumzika, GNM watakuelekeza masoko mbalimbali yaliyopo nchini China kulingana na mahitaji unayohitaji, kama unataka masoko ya nguo, utapelekwa kwenye masoko kama Yulong, Wantong, Canan, Liuhua, Shahe au Huimei kulingana na mahitaji yako.

 

Kama unahitaji masoko ya saa na urembo, utapelekwa kwenye masoko ya Zhanxi, Meibo au Xijiao na kama unahitaji masoko ya viatu, utapelekwa International Shoes Market Centre, Daxin Lu au Jiulong. Pia utapelekwa kwenye masoko ya bidhaa mbalimbali kama vifaa vya simu, vitambaa na mapazia, marumaru, handbags na samani za ndani za kila aina.

 

Utapewa mtu wa kuongozana naye ambaye atakusimamia katika manunuzi yako yote na kukuelewesha mitaa yote ya kupita na kukurudisha hotelini.

 

Baada ya kuwa umeshanunua mzigo unaoutaka, GNM pia watakusaidia kuufungasha vizuri mzigo wako, kuanzia ‘parcels’ ndogondogo kama mabelo ya nguo na viatu, mpaka parcels kubwa zinazohusisha makontena.

 

Baada ya hapo, utatakiwa kulipia gharama za kusa_irisha mzigo kuja Tanzania kisha wao watakusaidia huduma zote za kuandaa nyaraka za kusafirishia mizigo mpaka za kuja kutolea mzigo wako bandarini!

 

Uzuri ni kwamba gharama zao ni nafuu sana na usalama wa fedha na mizigo yako ni kwa asilimia 100! Kama wewe ni mfanyabiashara na kwa kipindi kirefu ulikuwa ukiogopa kusafiri kwenda China, GNM wanakuhakikishia usalama wako na mali zako kwa bei nafuu kabisa! Unasubiri nini?

 

Unaweza kuwasiliana nao kwa kufika Kariakoo jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Msimbazi, Mkabala na Benki ya Azania na Jengo la Simba Sport Club, ghorofa ya tatu au unaweza kuwapigia simu kwa namba 0677 066 551 au 0677 066 555.

 

Kwa nchini China, unaweza kuwasiliana na ofisi zao zilizopo Guangzhou kwa simu namba +86 138 297 21527 au +86 29721572.

Unaweza pia kutembeleawebsite yao kwa kubofya www.gnmtrading.com au watumie barua pepe kwa anuani ya info@gnmtrading.com au gnmtradco@yahoo.com .

 

MWANDISHI WETU
Toa comment