The House of Favourite Newspapers

SAFU YA UVCCM ‘KAMA YOTE’ YATEMBELEA GLOBAL

Viongozi wa UVCCM wakiwa katika picha ya pamoja na Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Amrani Kaima (wa kwanza kulia) na Mhariri wa Gazeti la Amani, Erick Evarist (wa pili kutoka kushoto).

 

VIONGOZI kutoka Idara tatu za Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM), UVCCM leo wametembelea Kampuni ya Global Publishers na kuweza kuona shughuli mbalimbali za uzalishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Risasi Jumamosi, Championi na Spoti Xtra.

Wakizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo ofisini kwake.

 

Viongozi hao waliongozwa na Katibu wa Uhamishaji na Chipukizi, Hassani Omary Bomboko, Katibu wa Siasa Oganaizesheni na Mahusiano ya Kimataifa, Peter Kasera, Katibu wa Vyuo na Vyuo Vikuu, Kamana Juma Simba na maofisa mbalimbali kutoka Makao Makuu ya CCM Taifa.

…wakipewa maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Usambazaji wa Global, Anthony Adam (wa kwanza kushoto).
Wakizungumza na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally ofisini kwake.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Hassani Bomboko, alisema mbali na kuona shughuli mbalimbali za uzalishaji wa magazeti, lengo la ziara hiyo pia ni kudumisha uhusiano mzuri kati ya UVCCM na Global kama chombo cha habari.

Katibu wa Uhamishaji na Chipukizi, Hassani Omary Bomboko (kulia) akiwa na ofisa kutoka Makao Makuu ya CCM, Juma Chikoka wakielekea Chumba cha Habari cha Magazeti Pendwa.
Mkuu wa Idara ya Global Digital, Edwin Lindege akitoa maelekezo kwa viongozi hao.

“Niwashukuru na niwapongeze kwa kufanya kazi nzuri, pokeeni pia salamu kutoka kwa mwenyekiti wetu wa Umoja wa Vijana, Kheri James ambaye amesema anatambua kazi kubwa mnayoifanya kupitia magazeti yenu ambayo yanaoongozwa kwa kusomwa na rika zote hususan vijana,” alisema Bomboko.

 

Na Mwandishi Wetu.

RC Dodoma ‘atumbua’ hadharani “Hatuna mzaha, mtapata tabu sana”

Comments are closed.