VIONGOZI kutoka Idara tatu za Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM), UVCCM leo wametembelea Kampuni ya Global Publishers na kuweza kuona shughuli mbalimbali za uzalishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Risasi Jumamosi, Championi na Spoti Xtra.
Viongozi hao waliongozwa na Katibu wa Uhamishaji na Chipukizi, Hassani Omary Bomboko, Katibu wa Siasa Oganaizesheni na Mahusiano ya Kimataifa, Peter Kasera, Katibu wa Vyuo na Vyuo Vikuu, Kamana Juma Simba na maofisa mbalimbali kutoka Makao Makuu ya CCM Taifa.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Hassani Bomboko, alisema mbali na kuona shughuli mbalimbali za uzalishaji wa magazeti, lengo la ziara hiyo pia ni kudumisha uhusiano mzuri kati ya UVCCM na Global kama chombo cha habari.
“Niwashukuru na niwapongeze kwa kufanya kazi nzuri, pokeeni pia salamu kutoka kwa mwenyekiti wetu wa Umoja wa Vijana, Kheri James ambaye amesema anatambua kazi kubwa mnayoifanya kupitia magazeti yenu ambayo yanaoongozwa kwa kusomwa na rika zote hususan vijana,” alisema Bomboko.
Na Mwandishi Wetu.
Comments are closed.