Saguda: Kamwe Sitaacha Kumposti Recho
MWIGIZAJI na mtayarishaji wa sinema za Kibongo, Saguda George amesema kati ya vitu ambavyo kamwe hawezi kuacha kuvifanya ni kumposti mitandaoni aliyekuwa mchumba wake, marehemu Rachel Haule ‘Recho’.
Akipiga stori na Susha Pumzi, Saguda alisema, licha ya kuwa ni miaka mitano sasa tangu Recho afariki dunia, lakini bado ‘anaishi’ kwenye moyo wake ndiyo sababu hasa amekuwa akifikisha hisia zake nje kwa watu wote.
“Siwezi kuacha kumposti Recho, ninapofanya hivyo ndiyo moyo wangu unakuwa na amani hivyo nitaendelea kumposti sana kwenye mitandao yangu ya kijamii,” alisema Saguda.
STORI: MWANDISHI WETU
Comments are closed.