The House of Favourite Newspapers

Sahle-Work Zewde Awa Rais wa Kwanza Mwanamke Ethiopia

Image result for Sahle-Work Zewde
Sahle-Work Zewde

BUNGE la Ethiopia limemchagua Sahle-Work Zewde kuwa rais wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo. Sahle-Work ni mwanadiplomasia mkongwe ambaye anakuwa mwanamke wa kwanza kuwa  mkuu wa nchi barani Afrika.

Kuchaguliwa kwake kunakuja baada ya wiki moja ambapo Waziri Mkuu,  Abiy Ahmed, ameteua nusu ya baraza lake la mawaziri wanawake.

Kushika kwake nafasi hiyo kumepokelewa kwa furaha na mitandao ya kijamii ya Ethiopia ikisema ni kitendo cha kihistoria, kinachokumbusha enzi za Malkia  Zewditu aliyeiongoza nchi hiyo mwanzoni mwa karne ya 20.

The new president standing with the prime miniser

Mbali na kushika nyadhifa kubwa kama msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais Sahle-Work pia ameiwakilisha Ethiopia kama balozi katika nchi za Senegal na Djibouti, alikuwa pia mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Umoja wa Afrika (AU).

 

Comments are closed.