The House of Favourite Newspapers

Said Salim Bakhresa Afika kutoa rambi rambi katika msiba wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania

Mmiliki wa Bakhresa Group, Said Salim Bakhresa (mwenye miwani ya rangi nyeusi) amefika kutoa rambi rambi katika msiba wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, nyumbani kwake Mikocheni, Dar Es Salaam.

Pichani Mzee Bakhresa yupo na Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi, ambaye ni mtoto wa hayati Ali Hassan Mwinyi.

Mazishi ya hayati Mwinyi yatafanyika Mangapwani, Zanzibar tarehe 02 Machi 2024.