Saint kumfungisha kizazi Kim Kardashian

26237E5B00000578-2971338-Kanye_West_and_Kim_Kardashian_pictured_leaving_a_Tattoo_Parlour_-a-3_1425032414657 Mwanamitindo Kim Kardashian.

Marekani
BAADA ya hivi karibuni Mwanamitindo Kim Kardashian kujifungua mtoto wa pili aitwaye Saint, madaktari wameshauri uzazi huo uwe wa mwisho lasivyo atajiweka kwenye hatari kubwa.

Imeelezwa kuwa, Kim mwenye umri wa miaka 35 alipomzaa North alipata matatizo yaliyohatarisha uhai wake lakini Mungu akajaalia akajifungua salama.

Wataalam wa afya wakasema kuwa, kitendo cha Kim kujifungua tena mtoto wa pili katika mazingiranhatarishi inamlazimu kuhitimisha kubeba mimba kama anajipenda.

Mtandao wa TMZ umeeleza kuwa, mtu wa karibu wa Kim ameweka wazi kuwa, Kim na Kanyen wanafanyia kazi ushauri wa madaktari na wamefi kia muafaka kwamba, Saint awe mtoto wa mwisho.

Loading...

Toa comment