The House of Favourite Newspapers

Sajenti Ampindua Johari Kwa Mtasha (Video)

Husna Sajenti akiwa na Mtasha.

MASTAA wetu bwana! Ndivyo unavyoweza kusema kufautia habari hii inayowahusu mastaa wa filamu Bongo, Husna Sajenti na Blandina Chagula ‘Johari’ ambao wanadaiwa kununiana kufuatia Sajenti kumpindua mwenzake kwa mwanaume mtasha.

 

Ilikuwa ni juzikati kwenye uzinduzi wa Filamu ya Sema uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar ambapo usiku mnene, Johari alionekana akiwa beneti na mtasha mmoja ambaye hakufahamika jina lake.

 

Kunaswa kwa wawili hao kuliwafanya ‘washakunaku’ waliokuwa ukumbini hapo wahisi staa huyo amejiokotea dodo chini ya muarobani hivyo baadhi kuanza kunong’ona wakisema ‘Johari kapata zali la mentali

 

Hata hivyo, tofauti na matarajio ya walio wengi, baada ya tukio la uzinduzi kumalizika, Sajenti alionekana akiondoka ukumbini hapo kwa madoido huku akiwa na Mzungu huyo, jambo lililowafanya wengi waone kuwa Johari kapinduliwa hivyo kuanza kuzomea.

“Ila na sisi kwa kupinduana hatujambo, hivi imekuwaje tena Sajenti anaondoka na yule Mzungu badala ya Johari, maskini Johari wa watu… ila siyo kesi kwa kuwa inaweza kuwa wamepeana kampani za kawaida tu,” alisikika akisema mdada mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.

Kufuatia tukio hilo, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Sajenti kuzungumzia mapinduzi ya kijanja aliyoyafanya kwa Johari lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa sms hakujibu.

Johari alipopatikana alikuwa na haya ya kusema: “Mimi ninachojua nilikutana na yule Mzungu, nikapiga naye picha kama ninavyopiga na watu wengine, hayo ya kupinduliwa siyajui, huyo Sajenti alitangulia kwenye gari wakati tunajipanga kuondoka na wala hatujanuniana chochote.”

Stori: Waandishi Wetu

Comments are closed.