Sajenti ataka wanaume wapigwe mawe!

MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Husna Iddi ‘Sajenti’ ameibuka na kueleza kuwa anatamani sheria ipitishwe kuwa wanaume wasiojua majukumu ya kulea watoto wao wapigwe mawe.  Sajenti ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, hilo ndilo dukuduku lake kwa wababa wanaozalisha akina dada kisha kutojua majukumu yao kama baba, jambo ambalo linawaumiza hivyo anatamani sheria kali ya wao kupigwa mawe ipitishwe.

“Unakuta mwanaume anamzalisha binti halafu baadaye anajifanya hajui majukumu yake, kwa nini asipigwe mawe? Sijui watunga sheria wako wapi watusaidie jamani maana suala hili linanikereketa sana,” alisema Sajenti ambaye amezaa na mwanamuziki Chaz Baba na Gabo Zigamba.


Loading...

Toa comment