The House of Favourite Newspapers

Sajuki Amliza Upya Wastara!

STAA wa Filamu nchini Tanzania, Wastara amesema inapofika tarehe kama ya leo  huwa anaikumbuka kwa kumuenzi aliyekuwa mume wake marehemu Juma Kilowoko Maarufu kama Sajuki.

 

Muingizaji huyo amesema huwa anaitumia siku ya leo kwa kuangalia picha za aliyekuwa mume wake ambaye na yeye pia  alikuwa mwigizaji wa filamu ambaye alifariki  Januari mbili katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mrefu.

 

Naweza nikawa nakosea sana lakini sina jinsi ni mapenzi ya dhati ndio yananituma kufanya hivi siwezi kuuzuia moyoUlipokuja kwenye maisha yangu kuna maisha mapya nimeishi na wewe na umeniacha nayo yawezekana yakawa yananitesa ama yananifariji lakini tu kuna kitu hakipo sawa tarehe 2/01 ndio siku uliyofariki na tar 01/ 01 ni siku ambayo sitaisahau,”ameandika Wastara kupitia ukurasa wake wa Instagram.

 

Aidha Wastara ameendelea kwa kuandika “Kama kupost picha zako kila mwanzo wa mwaka huwa kunaniletea shida na matatizo katika maisha yangu basi wacha tu yanikute niko tayari kuyapokea lakini hakuna wa kusitisha zoezi hili katika maisha yote mpaka nakufa mwaka mpya nitakuwa na wewe kokote niendapo japo kiroho inanitosha na kujiona tupo pamoja kwa siku chache ukinipa ile furaha uliyoondokana nayo. Mungu akupe kauli thabiti akuondosheee adhabu na mchanga mzito kaburini kwako”

Comments are closed.