The House of Favourite Newspapers

Sakata la Acacia, Bangi Vyawaweka Matatani Wabunge Wawili wa Mara

0
John Heche.

 

Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche anashikiliwa na Jeshi la Polisi Tarime, huku Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko naye akisakwa.

John Heche amekamatwa na kushikiliwa na Jeshi hilo kwa madai alizungumza bungeni kuhamasisha wananchi kuzuia shughuli za kampuni ya ACACIA huko Nyamongo, North Mara.

 

Esther Matiko.

 

Jeshi hilo pia linadai Heche kupitia mkutano wa hadhara alisema atapeleka hoja bungeni ili bangi ihalalishwe kuuzwa nje ya nchi, Polisi wanasema kauli hiyo inachochea ulimaji bangi.

Halikadhalika linamsaka Esther Matiko ili kumuunganisha katika madai hayo kuwa alizungumza katika mkutano huo kauli zinazochochea kilimo cha bangi.

Polisi wamechukua simu za alizokuwa nazo, pia wameagiza simu nyingine iliyopo Dar es salaam kwenye matengenezo pia ipelekwe Tarime.

-Makene

Rais Magufuli Alivyompokea Rais Museveni wa Uganda Jijini Tanga

Leave A Reply