Sakata la Bil. 20 Simba, Kigwangala Amsamehe Mo

 

ALIYEKUWA Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangala, leo Novemba 20, 2020,  kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram amesema  amemsamehe mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, baada ya kutokuwepo kwa maelewano baina yao, hali ilisababisha kuanza kurushiana maneno katika mitandao ya kijamii.

 

“Wanasimba tunataka ushindi dakika 90 uwanjani na mchango wa Mohammed siyo wa kudharau kwenye hili, lakini hata yeye na biashara zake wanafaidika na Simba as a brand, siyo bure tu.

 

Kigwangala ambaye ni mnazi wa Wekundu wa Msimbazi, ameendelea kuandika kuwa  thamani ya Simba siyo majengo, ni brand yenye umri wa zaidi ya miaka 80 Tanzania, ni lazima uwe Simba ama wale wengine hata kama unamiliki timu yako  siyo kitu kidogo Simba ina maslahi ya umma”.

 

“Ninaweza kusema mengi lakini siyo lengo langu, nimekuwa nikiwaza juu ya kusameheana  yaishe, tusonge mbele.  Naomba radhi kwake na kwa washabiki wote wa Simba niliowakwaza, mimi nimesamehe maisha yaendelee,”ameandika Kigwangala.

 

Chanzo cha ugomvi wao inaaminika kuwa ni Kigwangala kudai kuwa amenyimwa  mkopo wa pikipiki,   hali iliyopelekea kuanza kuhoji  uwekezaji wa Sh. bil. 20  ambazo Dewji aliziahidi kuwekeza Simba ambazo bado alikuwa hajaziweka.

Toa comment