The House of Favourite Newspapers

SAKATA LA DIAMOND LAMUIBUA DINNO

Diamond Platnumz

SAKATA la msanii mkubwa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kurekodi video chafu na kuziachia mtandaoni na kusababishia ‘msala’ kwa serikali mpaka akakamatwa na polisi, limemuibua msanii chipukizi wa muziki huo, Abdallah Manyuti ‘Dinno’ ambaye ametoa neno kwa staa huyo.

D Manyuti ‘Dinno’

Akipiga stori na Mikito Nusu Nusu, Dinno alisema tangu alipoingia kwenye muziki 2012 kipindi hicho akiitwa D Manyuti amekuwa akimtazama Diamond kama ‘role model’ wake na yeye ndiye aliyemvutia kufanya kazi na maprodyuza kama Sheddy Clever na wengineo ndiyo maana hata kazi yake mpya iitwayo Bado aliyoiachia hivi karibuni, ina vionjo kama vya Diamond, lakini matendo yake ya sasa yanamshangaza sana.

Dinno

“Nimekuwa nikimtazama kama nembo ya mafanikio kwa vijana kupitia muziki, naamini ipo siku na mimi nitafika levo zake lakini matendo yake ya sasa kwa kweli yananisononesha, namuombea kama kuna tatizo mahali, Mungu amfanyie wepesi lipite,” alisema Dinno ambaye anasimamiwa na lebo ya Nambiza Entertainment.

Comments are closed.