Kartra

Sakata la Kagere Kusepa Simba Lipo Hivi

IMEKWISHA hiyo! Ndivyo utakavyoweza kusema sasa rasmi mshambuliaji wa Simba Mnyarwanda, Meddie Kagere ataendelea kusalia katika klabu hiyo kwa msimu ujao.


Hiyo ikiwa ni siku chache tangu
tetesi zizagae za mshambuliaji huyo kutaka kutolewa kwa mkopo kwenda Klabu ya APR ya nchini Rwanda.

 

Pia awali ilielezwa mshambuliaji huyo aliandika barua kwa uongozi akiomba kuvunjiwa mkataba wake ili awe huru kwenda kukipiga kwingine.

 

Akizungumza na moja ya radio hapa nchini, Mshauri Mkuu wa C.E.O wa klabu hiyo, Crescentius Magori alisema kuwa hawana mpango wa kumuacha Kagere, hivyo bado ataendelea kuwepo hapo.

 

Magori alisema kuwa: “Meddie Kagere Bado yupo Simba, hatuna mpango wa kumtoa kwa mkopo.“Taarifa za Kagere kwenda kuitumikia kwa mkopo APR ya Rwanda si za kweli. Kwani bado anahitajika na kocha katika kuelekea msiju ujao.

 

“Kagere watu wanamchukulia poa, sio mtu wa kumchukulia poa, yupo na ataendelea kuwepo Simba.”


Toa comment