The House of Favourite Newspapers

Sakata La Kujitenga, Jela Yamuita Kiongozi Wa Catalonia

0
Kiongozi wa Catalonia aliyekuwa kinara wa vuguvugu la kujitenga, Carles Puigdemont.

SIKU chache baada ya Mahakama ya Kikatiba ya Hispania kutoa maamuzi ya kutupilia mbali maombi ya Catalonia kujitenga kutoka Hispania na kuwa taifa huru, kiongozi wa Catalonia aliyekuwa kinara wa vuguvugu la kujitenga, Carles Puigdemont anatafutwa na jeshi la polisi nchini humo kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka ya uhaini.

 

Puigdemont aliikimbia nchi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita na inaelezwa kwamba anapewa hifadhi ya kisiasa nchini Ubelgiji, baada ya mpango wake wa kujitenga kufeli vibaya kutokana na wakazi wa Catalonia kupiga kura kuukataa mpango huo.

 

Maandamano ambayo katika wiki kadhaa za awali yalikuwa yakiishinikiza Serikali ya Hispania kuipa uhuru Catalonia ili itambulike kuwa nchi huru, sasa yamebadilika na wananchi wanaandamana kwa amani wakiitaka Hispania iendelee kuwa taifa moja lenye nguvu na tayari maafisa wa serikali wameingia Catalonia na kukaa kweye vitengo vyote muhimu, ili kuzuia uwezekano wa kufanyika tena njama za kujitenga.
Kesi

Leave A Reply