The House of Favourite Newspapers

Sakata la Kutelekezwa Watoto, Wabunge Wamjia Juu RC Makonda – Video

Mbunge wa Ulanga Gudluck Mlinga ameitaka Wizara ya Katiba na Sheria kutoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na zoezi linaloendeshwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda la kuwatambua wakina baba waliowatelekeza watoto wao.

 

Akitoa hoja hiyo wakati wa kuchangia Bajeti ya Waziri wa Katiba na Sheria Mlinga amesema zoezi linaoendelea jijini Dar es Salaam linadhalilisha watu na halina staha katika jamii.

 

Aidha, baadhi ya wabunge wakapata fursa ya kuchangia hoja ya Mlinga na kutoa tahadhari. Waziri wa katiba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakapata fursa ya kujibu hoja hizo za wabunge

Comments are closed.