The House of Favourite Newspapers

Sakata la Lissu na Ben Saanane Laibuka Upya Bungeni, Waziri Mkuu Atoa Tamko (Video)

0
Tundu Lissu akiwa Hospitali ya Nairobi

 

Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni

Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkutano wa Tisa leo umeendelea mjini Dodoma ambapo katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu, Kassim Majaliwa, sakata la kushambuliwa kwa Tundu Lissu na kupotea kwa Ben Saanane liliibuka upya na kuzua mjadala mkubwa bungeni.

 

Swali kutoka kwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe, akitaka kujua serikali imechukua hatua gani mpaka sasa kufuatia sakata la kupotea kwa Ben Saanane na kushambuliwa kwa Tundu Lissu na serikali inatoa kauli gani kuhusu matukio hayo?

 

Akijibu swlai hilo, mheshimiwa waziri mkuu alisema ni kweli kwamba kumekuwa na matukio mengi ya ukatili na uvunjaji wa amani, si kwenye siasa tu bali kuanzia ngazi za familia mpaka taifa, akitolea mfano mauaji yaliyotikisa Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

 

Akaongeza kwamba serikali inaendelea na uchunguzi wa wahusika wa matukio yote hayo na pale uchunguzi utakapokamilika, serikali itatoa taarifa na kuwataka watu wote waendelee kujenga imani kwa vyombo vya usalama kwani vinaendelea vyema na kazi yao.

 

Mbowe alipopewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, aliendelea kupigilia msumari kwenye sakata la Lissu na kuhoji kwa nini wapelelezi kutoka nje ya nchi wasiite ili kufanyakazi hiyo? Waziri mkuu akasema suala hilo liachwe kwa vyombo vya dola vya ndani kwa sababu vinao uwezo wa kufanya kazi hiyo.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply