The House of Favourite Newspapers

Sakata la Madawa Bado Bichi, Wema, TID Kulala ‘Ndani’ Tena Leo

DAR: SAKATA la dawa za kulevya bado linaendelea hapa Dar es Salaam, ambapo leo Februari 6, 2017, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro  akizungumza na waandishi wa habari ametoa takwimu ya kilichofanyika ndani ya siku tatu tangu Ijumaa iliyopita.

Kamishna Simon Sirro amezungumza haya; “Tunaendelea vizuri na Oparesheni yetu ya kupambana na dawa za kulevya, tumekamata jumla ya watuhumiwa 112 na jumla ya kete 299 zidhaniwazo kuwa ni dawa za kulevya, kwa kawaida tutazipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na atatuambia ni aina gani.

Kamanda Sirro akizungumza na wanahabari leo

Kati ya watuhumiwa 112 ni watuhumiwa 12 tumewapeleka leo Mahakamani sababu sheria ya mwenendo wa mashtaka iko wazi, huwa inaturuhusu kuomba kuwaombea watuhumiwa kwa kiapo kwa hakimu, wawe chini ya uangaliazi wa Jeshi la polisi na Mahakama kwa muda wa miaka miwili wasifanye makosa tena.

“Wote tuliowakamata wengine wanakiri na wamekwenda kuonyesha hizo dawa za kulevya, kusudio la kwanza ni wawe chini ya uangalizi wetu na kusudio la pili la kiapo chetu ni waache hiyo tabia wawe raia wema, kusudio la tatu wawe wanakuja kuripoti kituo cha polisi angalau mara mbili kwa mwezi…. lengo letu ni kuona je wameacha kutumia dawa za kulevya?” – Kamishna Simon Sirro alisema.

Wema alivyoripoti Police Central, Ijumaa iliyopita.

Baada ya taarifa hiyo ya Sirro mwanahabari wetu aliondoka moja kwa moja kuelekea Mahakamani Kisutu kwa ajili ya kufuatilia nini kingejiri lakini taaraifa zilieleza kuwa ‘binding order’ ombi la kisheria la watuhumiwa hao ilicheleweshwa kupelekwa mahakamani, hivyo ikaelezwa kuwa  watapelekwa kesho asubuhi.

Kutokana na hivyo, wasanii Wema, TID, Lulu Diva na wengine waliokamatwa kwa tuhuma hizo wataendelea kusota sentro mpaka kesho watakapofikishwa mahakamani.

Comments are closed.