The House of Favourite Newspapers

Sakata la Spika vs CAG, Kumekucha Mahakamani, Zitto, Karume Waliamsha – VIDEO

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amemwandikia barua Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu kumtaka ashughulikie suala la Mahakama Kuu kukataa kupokea shauri la Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na wabunge wanne wa upinzani la kupinga Spika Ndugai kumuita CAG Prof. Mussa Assad.

 

Hayo yamesemwa leo na Zitto pamoja na Mwanaharakati wa masuala ya sheria na haki za binadamu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Fatma Karume wakati wakizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam;

 

“Mahakama Kuu Dar es Salaam imekataa kupokea Shauri letu la kikatiba kutaka tafsiri ya Katiba na Sheria zetu Kuhusu mamlaka ya Spika wa Bunge kumwita na kumshtaki Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali bila kujali Kinga ya Kikatiba ya CAG. Tumemwomba Jaji Mkuu aingilie.

 

“Sababu namba mbili ya Msajili wa Mahakama Kuu kukataa kupokea kesi yetu (admission) ni mtego wa kutaka kuona kama CAG anatutumia sisi kufungua kesi na hatutaingia mtego huo kwani hilo ni jambo la kujadiliwa mbele ya majaji na sio suala la kuamua kesi kupokelewa na kusajiliwa.

 

“Tunashuhudia kwa mara ya kwanza (labda) Mahakama inaangalia ushahidi kama kigezo cha admission ( usajili) wa kesi. Ushahidi unaopaswa kutolewa mahakamani unazuia kesi kusajiliwa. Yani Mahakama inasema kuwa ‘Spika hajamwita CAG mbele ya Kamati ya Maadili’.

 

“Mahakama inapozuia kesi KUSAJILIWA Ndipo unagundua kuwa nchi yetu imefika mahala pabaya sana. Obstruction of Justice hufanyika kwenye nchi zinazoongozwa na magenge ya kihalifu (GANGSTERS),” alisema Zitto.

WASIKIE ZITTO NA KARUME WAKIFUNGUKA

Comments are closed.