The House of Favourite Newspapers
gunners X

Sakata la Ubaguzi, Mabalozi wa Afrika Wakutana na Serikali ya China

0

MABALOZI wa Nchi za Afrika wamekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje China, Chen Xiaoding kuzungumzia changamoto zinazowakabili baadhi ya raia wa Afrika katika mji wa Guangzhou. Chen amewaeleaza Mabalozi kwamba Serikali ya China haiungi mkono vitendo vya ubaguzi dhidi ya yeyote.

 

Kuhusu changamoto zilizowasilishwa na Mabalozi wa Nchi za Afrika zinazowakabili Waafrika nchini China, China imesema Mamlaka ya Jimbo la Guangdong itachukua hatua kuzishughulikia ikiwemo Raia wa Afrika ambao wameondolewa kwenye makazi na hoteli kupatiwa makazi mbadala ya muda. Hatua hizo ni pamoja na;

 

1) Kuhakikisha kwamba zoezi la udhibiti wa Maambukizi ya COVID19 linaendeshwa kwa usawa bila kulenga kundi mahususi la kijamii;

2) Raia wa nchi za Afrika ambao wameondolewa kwenye makazi na hoteli kupatiwa makazi mbadala ya muda;

3) Kutoa elimu kwa umma hususan kwenye maeneo ya huduma na katika Jamii juu ya kuepuka hatua zozote zinazoweza kutafsiriwa kuwa ni ubaguzi dhidi ya kundi lolote la kijamii.

 

4) Kuanzisha mtandao mahususi wa mawasiliano kati ya Mamlaka ya Jimbo la Guangdong na Ofisi za Kibalozi zilizopo katika jiji la Guangzhou kwa ajili ya kushughulikia kwa haraka changamoto zozote zitakazojitokeza.

 

Aidha, China imewaahidi Mabalozi wa Nchi za Afrika kuwa itahakikisha zoezi la udhibiti wa corona linaendeshwa kwa usawa, kutoa elimu kwa umma ili kuepuka hatua zinazoweza kutafsiriwa kuwa ni ubaguzi na Kuanzisha mtandao wa mawasiliano kati ya Mamlaka za Nchi hiyo na Ofisi za Kibalozi.

 

Chen amewaeleaza Mabalozi kwamba Serikali ya China haiungi mkono wala kuridhia vitendo vya Ubaguzi dhidi ya mtu yoyote. Na inathamini mahusiano yake na Mataifa ya #Afrika katika majira yote.

 

“Ubalozi utaendelea kuwasiliana na Jumuiya ya Watanzania waliopo Guangzhou ili kupata mrejesho wa hali halisi inavyoendelea katika jiji la Guangzhou. Aidha, Ubalozi unatoa rai kwa Watanzania wote waliopo China kuendelea kutiii Sheria za Nchi hususan zinazohusu udhibiti wa COVID19.

Leave A Reply