The House of Favourite Newspapers

Sakata la Umeya Dar: Saed Kubenea apandishwa kizimbani leo

0

kubeneaMbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.

MBUNGE wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) pamoja na Diwani wa Kimanga Manase John Mjema wamepandishwa kizimbani leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar na kusomewa shtaka la kumjeruhi Theresia Mbaga kwenye ukumbi wa Karimjee mnamo Februari 27 mwaka huu.

Mmbando alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika kwenye Ukumbu wa Kareem Jee na baadaye kuahirishwa hatua ambayo iliibua malumbano.
Mbele ya Cyprian Mheka, Hakimi Mkazi Kisutu washitakiwa hao walikana kosa hilo ambapo hakimu alighairisha kesi hiyo mpaka tarehe 16 Machi mwaka huu.

Kubenea na Mjema wote wamekana shtaka na kujidhamini wenyewe baada ya kusaini dhamana ya shilingi milioni mbili kila mmoja.

Washtakiwa wengine katika shtaka hilo ni Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima James Mdee, Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mwita Mwikabe Waitara na wengine wawili.

Jana asubuhi kwenye mahakama hiyo Kubenea akihudhuria kesi yake dhidi ya Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, alikamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa chini ya ulinzi.

Leave A Reply