Sakho, Mugalu Kuwakosa Waswana
NYOTA wawili wa Simba kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, na mshambuliaji Chris Mugalu wanatarajiwa
kukosekana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy, kutokana na
programu ya mapumziko waliyopewa na timu ya madaktari wa timu hiyo.
Sakho na Mugalu wote walipata majeraha yao katika mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma
Jiji. Simba walishinda 1-0.
Nyota hao wawili Jumanne walikosekana katika mazoezi ya Simba yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy
ya Botswana, keshokutwa Jumapili.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Daktari wa viungo na mchua misuli wa Simba, Fareed Caseem, alisema:
“Tunatarajia kuendelea kuwakosa wachezaji wetu wawili, ambao ni Pape Ousmane Sakho ambaye alipata majeraha ya kifundo cha mguu na amepewa siku kumi za mapumziko, huku mshambuliaji Chris Mugalu yeye akiwa amepewa wiki tatu za mapumziko.”
Kocha Didier Gomes ataendelea kukosekana kwenye mechi za kimataifa kutokana na kutokuwa
na vigezo vya Caf huku Selemani Matola naye akiwa masomoni, hivyo Simba itaongozwa na Mnyarwanda, Thierry Hitimana