Salah Atawazwa Mchezaji Bora wa Afrika wa Caf 2018

Mshambuliaji wa Misri na klabu ya Liverpool ya England, Mohamed Salah, ndiye Mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kwa mwaka 2018.  Hii  ni mara yake ya pili kushinda tuzo hiyo. Salah, 26, alimshinda mwenzake wa Liverpool, Sadio Mane, kutoka Senegal na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.

Alikabidhiwa tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika nchini Senegal, Jumanne wiki hii.

“Nimekuwa na ndoto ya kushinda tuzo hii tangu nilipokuwa mdogo na sasa nimefanya hivyo mara mbili mfululizo,” Salah alisema.

Mshambuliaji wa Houston Dash kutoka Afrika Kusini, Thembi Kgatlana, alitawazwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Kike.

Salah pia alitawazwa Desemba mwaka jana Mwanakandanda Bora wa Mwaka wa Afrika wa shirikisho la utangazaji la Uingereza (BBC) kwa mara ya pili mfululizo.

Aliwafungia Liverpool mabao 44 msimu wa 2017-18 na kuisaidia klabu hiyo kufika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ingawa walishindwa na Real Madrid. Aidha, alifunga mabao mawili akichezea Misri katika Kombe la Dunia nchini Urusi. Amefunga mabao 16 katika mechi 29 alizoichezea Liverpool mashindano yote msimu huu.

Salah, Mane na Aubameyang wamo kwenye Kikosi Bora cha Mwaka Afrika  na beki wa Manchester United Eric Bailly, kiungo wa kati wa Manchester City Riyad Mahrez, kiungo wa kati wa Liverpool Naby Keita na beki wa kushoto wa Tottenham Serge Aurier.

Jumanne wiki hii, Caf ilitangaza pia kwamba Misri itakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 baada ya Cameroon kushindwa kujiandaa kwa wakati.

Kikosi Bora cha Afrika XI: Denis Onyango (Mamelodi Sundowns/Uganda), Serge Aurier (Tottenham/Ivory Coast), Medhi Benatia (Juventus/Morocco), Eric Bailly (Manchester United/Ivory Coast), Kalidou Koulibaly (Napoli/Senegal); Naby Keita (Liverpool/Guinea), Thomas Partey (Atletico Madrid/Ghana), Riyad Mahrez (Manchester City/Algeria); Mohamed Salah (Liverpool/Misri), Pierre-Emerick Aubameyang (Arsenal/Gabon), Sadio Mane (Liverpool/Senegal).

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment