The House of Favourite Newspapers

Salasala, Tegeta, Bunju huwaambii kitu kwa Betika

WASOMAJI wa Gazeti la Betika maeneo ya Salasala, Tegeta na Bunju jijini Dar es Salaam, huwaambii kitu kuhusu Gazeti la Betika baada ya kusema kwamba gazeti hilo kwa sasa ndiyo kiongozi wao kwenye masuala ya kubeti.

Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, limekuwa likitolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 ambapo lina kurasa 20 ambazo zote ni za rangi.

Gazeti hilo linaloingia mtaani kila Jumatano, linajihusisha na masuala ya kubeti ambapo ndani yake kuna makala na takwimu za mechi mbalimbali.

Leo Jumatano, timu ya Maofisa Masoko ya Global Publishers, ilitembelea mitaa hiyo ya Salasala, Bunju na Tegeta na kukutana na wasomaji kadhaa waliotoa maoni yao juu ya gazeti hilo.

“Sijui niseme nini juu ya hili gazeti kwani kwa sasa ndiyo limekuwa kiongozi kwangu katika masuala ya kubeti.

“Tunawapongeza kwa kulileta gazeti hili lenye makala na uchambuzi mbalimbali wa mechi ambao unatusaidia katika kubeti.

“Betika limekuwa gazeti la kwanza hapa nchini kuja kivingine kwani kuna magazeti mengi, lakini hili kwanza linatolewa bure, pia linajihusisha na masuala ya kubeti pekee kitu ambacho kwa sasa hapa nchini kimeshamiri,” alisema Paulo Joseph ambaye ni mkazi wa Tegeta.

Kwa upande wa Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisisitiza kwamba, lengo kubwa la Betika ni kumfikia kila Mtanzania katika pande zote za nchi na wao kama timu, watahakikisha wanafika popote pale kwenye makazi ya watu.

“Wasomaji wetu tunawajali sana, kila siku tumekuwa tukiweka vitu vizuri ndani ya gazeti letu hili ambalo huwa tunalitoa bure.

“Tumejipanga kuhakikisha tunafika kila sehemu ambapo kuna makazi ya watu, kubwa zaidi ni kuwafikishia hili gazeti ambalo lina maujanja mengi ya kubeti.

“Pia bado tunapokea matangazo, hivyo hii ni fursa ya watu ambao wanataka kutangaza nasi kuleta matangazo yao kwetu, tunawakaribisha ofisini kwetu Sinza Mori jijini Dar,” alisema Mgema.

Comments are closed.