Saleh Ally: Yanga Haina Kikosi Bora na Haina Kikosi Kipana – Video

Mchambuzi wa Soka kutoka katika kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na 255globalradio na Global TV Saleh Ally ‘Jembe’

MCHAMBUZI wa soka kutoka kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na 255globalradio na Global TV Saleh Ally maarufu kama Jembe amesema mashabiki wa soka hasa wa klabu ya Yanga waache kujidanganya klabu ya Yanga haina Kikosi Bora na haina kikosi kipana kama ambavyo watu wanadhani.

 

Jembe ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ubora wa Yanga ukilinganishwa na ubora wa Simba wa miaka ya hivi karibuni ambao umeifanya Simba itawale soka la Tanzania kwa kipindi cha miaka mnne mfululizo.

 

Katika maelezo yake Jembe amesema Simba ndiyo timu bora kutokana na kufanya vizuri kwa muda wa miaka minne mfululizo katika ngazi ya soka la ndani lakini pia kupata mafanikio katika michezo na mashindano ya kimataifa ikiwemo Ligi ya Mabingwa Barani Afrika pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

 

Jembe anaamini Yanga bado inapitia kipindi cha mpito au mabadiliko(Transition Period) ambayo inatoka katika hatua ya mabadiliko ya timu ambayo ilikuwa inatengenezwa inaenda katika hatua ya kuanza kuchukua mataji na kuwa bora.

 

“Yanga ni ile timu iliyotoka kwenye Transition misimu miwili nyuma tulikuwa tunawaambia timu bado wao wanasema tayari.” alisema Jembe.

Mchambuzi wa Soka Saleh Ally ‘Jembe’

Alipoulizwa kuhusu timu bora ni ipi alijibu:

“Timu bora ni mfano wa Simba kwa Tanzania ambayo imefika robo fainali ya mashindano ya kimataifa mara tatu ndani ya misimu mine, katika michuano mikubwa Barani Afrika, Imechukua Ubingwa wa Nchi mara nne, imechukua ubingwa wa Shirikisho mara mbili, ngao za jamii mara nne nafikiri unaweza kuona hizo takwimu.”

 

Mchambuzi huyu mkongwe amebainisha kuwa Simba ndiyo mfano wa Timu Bora ambayo imefanikiwa kuchukua makombe manne ya Ligi Kuu Bara, imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali mara tatu ya mashindano ya kimataifa.

 

Simba na Yanga zinatarajiwa kuumana katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports kesho Mei 28 majira ya saa kumi jioni.

YANGA Yapata PIGO ZITO Kuelekea DERBY, CLATOUS CHAMA Kuikosa DERBY MWANZA | SPORT ZONE..3470
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment