The House of Favourite Newspapers

Samatta Ampa Mchongo Msuva Ulaya

 MSHAMBULIAJI wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta, amempa ‘mchongo’ kiungo mshambuliaji wa Difaa El Jadida ya Morocco, Simon Msuva kuhakikisha anayafikia malengo aliyojiwekea ya kusonga mbele zaidi katika soka kwa kuondoa vile vitu vinavyomfanya asifanye vyema na kujiboresha zaidi.

 

Samatta kwa sasa ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu ya Ubelgiji kwa kuwa na mabao 10 huku akielezwa kuwa anazivutia timu kadhaa kutoka Eng­land ikiwemo Everton, West Ham United na Leicester City, hivyo amemuonyesha mlango wa kupitia Mtanzania mwenzake huyo.

Akizungumza na Cham­pioni Ijumaa, Msuva alisema Samatta amekuwa akim­sihi na kumuelekeza mara kadhaa juu ya kuendelea kujituma na kujiimarisha ili aweze kuwa bora zaidi.

“Nimefurahishwa na kasi ya Samatta kama kaka yangu aliyenitangulia katika safari ya soka la kulipwa na mimi ndiyo kwanza nina mwaka mmoja, amekuwa mshambuliaji mzuri ambaye kwake kumalizia ndiyo kila kitu jambo ambalo ndivyo mshambuliaji anavyotakiwa kuwa.

 

“Tumekuwa tukiwasiliana mara kwa mara na kun­ieleza vitu vingi vya kufanya kwa kuangalia jinsi ninavyocheza huku akiniele­keza baadhi ya vitu kuacha na vingine kuvi­ongezea pindi ninapokuwa uwanjani ili ni­weze kuimarisha kiwango changu kiwe bora na kufikia mafanikio, jambo ambalo nalifanyia kazi,” alisema Msuva.

 

Msuva alijiunga na Difaa Julai, mwaka jana akitokea Yanga kwa dau la dola 100,000 (Sh 222m) na kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji tegemeo ndani ya kikosi chake.

Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Jokate Mwegelo Alivyowapandisha Madenti kwenye Ndege

Comments are closed.