The House of Favourite Newspapers

Samatta Ampeleka Mkewe Ubelgiji

0

NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na mshambuliaji wa KR Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, ameamua kumbeba jumla mkewe kwa kumpeleka Ubelgiji.

 

Samatta alifunga ndoa na mzazi mwenzie, Neima Magange, Oktoba 10, mwaka huu maeneo ya Mtoni Kijichi jijini Dar, ndoa ambayo ilikuwa ya kimyakimya huku wakitarajia kufanya sherehe baadaye.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, baba mzazi wa nyota huyo, Mzee Samatta amefunguka kuwa, nyota huyo ameamua kuondoka na mke wake ili kuweza kuendelea na maisha mengine.

“Samatta ameamua kumchukua mkewe kwenda naye Ubelgiji ambapo wanaendelea na maisha yao, alim

chukua kipindi kile alipokuja kucheza mechi ya kimataifa dhidi ya Libya, hivyo alivyoamua kuondoka ameondoka na mkewe.

 

“Nadhani anatarajia kurejea huku hivi karibuni katika likizo za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya,” alisema mzazi huyo.

Leave A Reply