Samatta Arejeshwa Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025, Kikosi Kipo Hapa
Kaimu Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Hemed Suleiman ‘Morocco’ ametangaza kikosi cha timu hiyo kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Oktoba 10, 2024 na Oktoba 15, 2024.
Katika kikosi hichi nahodha wa Stars, Mbwana Samatta amerejeshwa kikosini huku kwa mara ya kwanza beki wa Simba Sc, Abdulrazack Hamza akiitwa kikosini.