STRAIKA namba moja kwa Tanzania na supastaa wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mtanzania Mbwana Samatta, ameingia kwenye orodha ya wachezaji 30 bora Afrika na kuwania tuzo pamoja na wakali kibao, Mohamed Salah na Sadio Mane.
Samatta ameweka rekodi ya kuingia miongoni mwa nyota watakaogombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika baada kutajwa na Shirikisho la Afrika (Caf). Hii ni kwa mara ya kwanza kwake kuingia katika kundi hilo.
Hii ni kwa mara ya kwanza kwa Samatta kuwania tuzo ya uchezaji bora Afrika akiwa nje ya bara hili ikiwa tayari ana tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji waliokuwa wanacheza ndani.
Kutajwa kwa nyota huyo kuwania tuzo hiyo sambamba na Mane na Salah, ni kutokana na mafanikio makubwa aliyokuwa nayo msimu uliopita akiwa Genk kwa kutwaa ubingwa wa ligi, kutwaa tuzo ya Ebony Shoe na kufunga mabao 23.
Straika huyo atawania tuzo hiyo sambamba na Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Arsenal), Riyad Mahrez (Algeria & Manchester City), Sadio Mane (Senegal & Liverpool) na Taha Yassine Khenissi (Tunisia & Esperance).
Wengine ni Thomas Teye Partey (Ghana & Atlético Madrid), Victor Osimhen (Nigeria & Lille), Wilfred Ndidi (Nigeria & Leicester City), Wilfried Zaha (Ivory Coast & Crystal Palace), Mohamed Salah (Misri & Liverpool).
Pia Moussa Marega (Mali & Porto), Naby Keita (Guinea & Liverpool), Nicolas Pepe (Ivory Coast & Arsenal), Odion Ighalo (Nigeria & Shanghai Shenhua), Percy Tau (Afrika Kusini& Club Brugge). Pia wapo Youcef Belaili (Algeria & Ahli Jeddah), Hakim Ziyech (Morocco & Ajax), Idrissa Gueye (Senegal & Paris Saint-Germain), Ismail Bennacer (Algeria & AC Milan), Jordan Ayew (Ghana & Crystal Palace), Kalidou Koulibaly (Senegal & Napoli), Kodjo Fo Doh Laba (Togo & Al Ain), Mahmoud Hassan ‘Trezeguet’ (Misri & Aston Villa), Baghdad Bounedjah (Algeria& Al-Sadd), Eric Maxim Choupo-Moting (Cameroon & Paris Saint- Germain), Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns), na Carolus Andriamatsinoro (Madagascar & Al Adalah).
Msimu huu tayari Samatta amefunga mabao mawili katika Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa) huku akifunga mabao sita katika Ligi Kuu ya Ubelgiji (Jupiler).
SAID ALLY, Dar es Salaam
Comments are closed.