The House of Favourite Newspapers

Samatta Awapiga Liverpool Bonge La Bao – Video

HATIMAYE mshambuliaji raia wa Tanzania, Mbwana Samatta, usiku wa kuamkia leo aliwapa mashabiki wa soka kile walichokuwa wanakitaka baada ya kufanikiwa kuifungia timu yake ya KRC Genk bao moja ilipopata kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Liverpool.

 

Mashabiki karibia nchi nzima Tanzania walikuwa kwenye televisheni zao wakiwa wanasubiri mchezo huo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ili kuona mshambuliaji huyo atafanya nini.

 

Wengi walikuwa hawasubiri matokeo, bali walitaka kumuona nahodha huyo wa Taifa Stars akiwafunga Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo baada ya kukutana nao kwenye mchezo wa kwanza, akafunga lakini VAR ikamgomea.

Mbwana Samatta akishangilia baada ya kufunga bao.

Samatta alikuwa akitamani mara kwa mara kuona anaifunga Liverpool ambayo inaongozwa na mabeki imara akiwemo Virgil van Djik ambaye alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya miezi kadhaa iliyopita. Katika mchezo huo, Liverpool walikuwa wa kwanza kujipatia bao kupitia kwaGeorginio Wijnaldum, katika dakika ya 13 tu  baada ya mabeki wa timu hiyo kufanya uzembe.

 

Hata hivyo, dakika ya 38 nusura Genk warudishe bao hilo kupitia kwa Samatta, lakini Van Djik aliugusa mpira na kuutoa nje. Dakika ya 40, Samatta alifanikiwa kuifungia timu yake bao safi  la kusawazisha baada ya kuuwahi mpira wa kona na kupiga kichwa safi  mbele ya James Milner kilichojaa wavuni moja kwa moja.

Hili ni bao lake la pili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu na anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza kwenye Dimba la Anfield na kufunga bao.

 

Liverpool waliamka kipindi cha pili na kufunga lingine kupitia kwa Alex Oxlade Chamberlain katika dakika ya 53. Sasa Liverpool wamefi kisha pointi tisa huku Genk wakiwa na pointi moja katika nafasi ya ya mwisho kwenye Kundi E.

 

Chelsea waamka baada ya kichapo Chelsea wakiwa nyumbani walikutana na dhahama kubwa baada ya kuchapwa mabao 4-2 hadi dakika ya 50 lakini wakamaliza mechi hiyo kwa sare ya 4-4 dhidi ya Ajax.

 

Katika mchezo huo, mabao ya Ajax yalitokana na Chelsea kujifunga mabao mawili kupitia kwa Tammy Abraham na Kepa, huku mengine yakifungwa na Promes na Van de Beek na Chelsea wakifunga kupitia kwa Jorginho aliyefunga mawili, James na Azpilicueta. Matokeo mengine Inter Milan walionja joto ya jiwe baada ya kuchapwa mabao 3-2 dhidi ya Borrusia Dortmund, Lyon wakaipiga Benfi ca mabao 3-1, Napoli na Salzburg wakatoka 1-1.

Comments are closed.