The House of Favourite Newspapers

Samatta hajachoka mleteeni hao Algeria

0

SAMATTA.jpg

Straika wa Taifa Stars, Mbwana Samatta.

Na Wilbert Molandi

STRAIKA wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amewatoa hofu Watanzania kwa kuwaambia hana uchovu wowote na atajituma kadiri ya uwezo wake kuipa ushindi Tanzania dhidi ya Algeria, leo Jumamosi.

Samatta12.jpgSamatta ataichezea Taifa Stars dhidi ya Algeria kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2018 akiwa ametoka kuipa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika klabu yake ya TP Mazembe ya DR Congo.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Samatta alisema kuwa yupo fiti kwa ajili ya mechi hiyo ya Algeria kutokana na maandalizi waliyoyafanya chini ya Kocha Charles Mkwasa.

Pia Samatta alisema, juzi jioni alikaa pamoja na wachezaji wenzake kwa ajili ya kuwapa morali na kuwatoa hofu ya mchezo huo ili kuhakikisa wanashinda nyumbani kabla ya kwenda kurudiana ugenini.

“Watanzania wengi wana hofu kuwa uhenda nikawa nimechoka na nikashindwa kucheza mechi ya kesho (leo) dhidi ya Algeria, kitu ambacho siyo sahihi.

“Ningependa kuchukua muda huu kuwatoa Watanzania kuwa nipo fiti kwa ajili ya mechi na Algeria, licha ya kucheza fainali wikiendi iliyopita ya michuano ya Afrika.

“Kikubwa nilichopanga mimi na wachezaji wenzangu ni kuipa sifa nchi yangu kwa kuhakikisha tunawafunga Algeria na kusonga mbele kwenye michuano hiyo,” alisema Samatta.

Leave A Reply