Samatta ni EPL tu wengine wasahau

BABA mzazi wa mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta, Mzee Ally Samatta atasimamia mwanaye atue ndani ya Ligi ya England na kuachana na ofa za nchi nyingine ambazo amezipata.

 

Samatta ambaye ndiye kinara wa mabao katika Ligi ya Ubelgiji amekuwa akihusishwa kutua katika klabu mbalimbali za England sambamba na Uturuki. Ofa ya juzi ni kutoka Cardiff City ambayo Genk waliipiga chini.

 

Akizungumza na Spoti Xtra linatoka Alhamisi na Jumapili, Mzee Samatta amesema; “Ninachotaka kuona ni kwamba Samatta anatua ndani ya nchi ya England na siyo kwingine ambapo wamekuwa wakimtaka wao aende.”

Loading...

Toa comment