The House of Favourite Newspapers

Samatta si wa Mchezo Mchezo, Aibeba Stars, Atupiamo Dakika 3 za Mwanzo na 3 za Mwisho

MSHAMBULIAJI wa anayeiwakilisha Tanzania Kimataifa kutoka Klabu inayocheza Ligi Kuu ya Ubelgiji na Europa League, KRC Genk, Mbwana Ally Samatta ameibeba Taifa Stars baada ya kuongoza jahazi na kufanikiwa kutupia bao mbili za kwake wakati Taifa Stars ikiichapa Botswana bao 2-0.

Katika mchezo huo wa kirafiki kwenye Kalenda ya FIFA uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Samatta alitupia bao hizo kunako dakika ya 3 na ya 87 ya mchezo huo huku akionesha kiwango bora cha soka.

TAZAMA VIDEO YA MABAO YOTE ALIYOTUPIA SAMATTA

Comments are closed.