The House of Favourite Newspapers

Samatta, Ulimwengu wakiwa benchi, Stars itapambana

0

urlThomas Ulimwengu.

MSHAMBULIAJI hatari wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Abdallah Kibadeni amesema inatakiwa washambuliaji wengine wa Taifa Stars wazidi kujituma hadi ifikie kuwa na kikosi hata kama Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wako benchi, bado timu iweze kujituma na kushinda.

http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/10/12oc13-tpma-fcmk_207_1381681076.jpg?resize=648%2C400

Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wakishangilia.

Kibadeni ambaye ni mshauri wa ufundi katika kikosi cha Taifa Stars amesema lazima washambuliaji wengine wajifunze kupitia Samatta na Ulimwengu ambao wanachezea kikosi cha TP Mazembe ya DR Congo.

“Wakati wa enzi zetu, kulikuwa na zaidi ya washambuliaji 10 hatari nchini. Ukiitwa Taifa Stars hauwezi kufanya utani, unajua nafasi yako kuna watu wengine wakali.

“Huo ndiyo mfumo mzuri wa kufanya timu ya taifa kuwa na kikosi kikali kutokana na ushindani wa juu wa namba.

“Vijana walio nyumbani wana uwezo, tatizo kubwa ni uzoefu lakini wao pia wanapaswa kujituma na kuamini kwamba kazi ni ngumu na mambo si rahisi.

“Stars iwategemee akina Samatta, lakini vizuri zaidi nao wawe tegemeo. Hata wale ambao watakuwa benchi basi wale walio nyumbani nao wacheze na kutoa mchango uleule,” alisema Kibadeni.

Taifa Stars imeweka kambi mjini Johannesburg kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria itakayopigwa Novemba 14, jijini Dar es Salaam.

Samatta na Ulimwengu, hawajajiunga na kambi hiyo kutokana na kubanwa na majukumu kwa kuwa TP Mazembe leo Jumamosi inacheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya USM Alger mjini Lubumbashi, DR Congo.

 

Leave A Reply