The House of Favourite Newspapers

#GlobalUpdates: Samsung Wanatuambia Wao Ndio Wa Kwanza Kuwa Na Upgrade Hii Kwenye Soko La Simu Duniani – (Video)

Moja kati ya habari zinazobamba kwenye mitandao leo Machi 30 2017 ni pamoja na toleo jipya la simu ya Samsung (The Galaxy Series) – Samsung Galaxy S8 na S8 Plus, na kama wewe ni mpenzi wa simu hizo kuna baadhi ya vitu muhimu vya kufahamu haswa kama wewe ni mtumiaji mkubwa wa kutuma, kupokea files na kusikiliza miziki kupitia Bluetooth.

Nimetembelea mtandao wa The Verge na kukutana na stori (habari) kuhusu toleo jipya la Samsung Galaxy S8 na S8 Plus. Kwa mujibu wa mtandao huo, toleo jipya la The Samsung Galaxy series S8 na S8 Plus ni simu ya kwanza kwenye soko la bidhaa za simu na vifaa vya kidigitali kuwa na upgrade mpya ya Bluetooth – Bluetooth 5.0 kutoka ile inayotumiwa sasa Bluetooth 4.2.

Mbali na upgrade hiyo, miongoni mwa faida za Bluetooth 5.0 ni pamoja na mabadiliko ya quality ya sauti, kasi ya connectivity kati ya devices na uwezo wa kukamata masafa marefu zaidi. The Verge imeendeleaa kuripoti kuwa Bluetooth 5.0 ina kasi mara mbili zaidi kuliko Bluetooth 4.2 na uwezo wa kuunganisha simu zaidi ya moja kwa umbali zaidi ya futi 800 (mita 240).

Kwa wale wanaopenda kusikiliza miziki na marafiki zao bila kuweka loudspeaker, Bluetooth 5.0 ina uwezo wa kushinikiza sauti kwenye seti mbili za wireless headphones kwa wakati mmoja hivyo hakutokuwa na haja ya kumuazima mwenzako siko moja la headphone ili kuzisikiliza ngoma mzipendazo kwa pamoja.

Kuhsuiana na bei, bado haijawekwa wazi simu hiyo itauzwa kwa bei gani ila Samsung wameahidi kutoka makadirio hayo kulingana na nchi tofauti very soon.

Tazama jinsi Samsung Galaxy S8 na S8 Plus ilivyo na jinsi utakavyoweza kuitumia na kuifadi hapa chini.


Kwa taarifa zaidi juu ya Samsung Galaxy S8 na S8 Plus, isogelee The Verge hapa kwenye hii link ya blue.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown

Source: The Verge.

Video: YouTube/The Verge.

 

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.