Samuel Eto’o Atua Bongo – Video

NAHODHA wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon, Klabu ya Barcelona na Chelsea, Samuel Eto’o tayari amewasili nchini Tanzania leo Oktoba 10, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Eto’o ambaye amealikwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager amekuja Tanzania kwa wajili ya kuzindua mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira aina ya 5-A-Side utakaojengwa Oyster Bay, Dar es Salaam.

TBL imeamua kujenga uwanja huo kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamiii ya Watanzania ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiwaunga mkono kibiashara.

Lengo la kumleta Et’oo nchini ni kuongeza  hamasa kwa wanamichezo wenye vipaji kujitokeza kushiriki katika soka na kutoa fursa kwa Watanzania ambao hawajawahi kumuona.

Uwepo wa Eto’o nchini utakuwa chachu kwa Watanzania kushiriki katika mchezo huo.

PICHA NA GLOBAL TV ONLINE

Toa comment