SAMUEL ETO’O Atua Nchini, Kufungua Mashindano Ya 5-Aside Kesho – VIDEO

Balozi wa Castle Africa 5s nchini Tanzania, Ivo Mapunda (kushoto) akiwa na Samuel Eto’o.

BALOZI  wa Castle Africa 5s nchini Tanzania, Ivo Mapunda  leo Juni 6, 2019 amewaongoza watanzania kumpokea  mshambuliaji wa zamani wa Cameroon na klabu kubwa Ulaya ikiwemo Barcelona, Inter Milan na Chelsea na Balozi wa Castle Africa 5s, Samuel Eto’o katika  Uwanja wa ndege wa Kimataifaa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na baada ya hapo aliondoka na msafara mpaka katika hoteli ya Lamada Mbezi ambapo ataongea na wanahabari.

Staa huyo ametua nchini kufungua mashindano mashindano ya Castle Lager yajulikanayo kama “Castle Africa 5s (5- aside) yatakayojumuisha timu nane kutoka nchi nane za Africa Tanzania ikiwa mwenyeji.

Fainali hizo zinatarajiwa kuanza kesho Ijumaa ya Juni 7,2019 katika Uwanja wa Uhuru zikiwakilishwa na timu ya Wanaume na Wanawake kutoka kila nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Bia ya Castle Lager nchini Tanzania, Pamela Kikuli alisema timu kutoka nchi saba zikiwakilishwa na timu ya Wanaume na Wanawake zinatarajia kuwasili pia leo alhamisi Juni 6,2019  ambapo zitapokewa kwa namna tofauti kwa kadri zitakavyokuwa zikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam pamoja na Balozi wa Castle Africa 5s, Samwel Eto’o.

Pamela alizitaja nchi shiriki katika fainali hizo kuwa ni Africa Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Lethoto, Uganda, wenyeji Tanzania na nchi alikwa ya Nigeria.

 

Kwa upande wa Mapunda alisema timu zimejiandaa vizuri kiushindani  na wameahidi ushindi utabaki Tanzania hivyo anaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kuja kushangilia timu zao.

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba, Faustina Charles (Nandy) na Rajabu Abdul (Harmonize) kukutana jukwaa moja katika Uwanja wa Uhuru kutoa burudani katika fainali za mashindano ya Castle Lager yajulikanayo kama “Castle Africa 5s (5- aside) yatakayojumuisha timu nane kutoka Nchi nane za Africa Tanzania tukiwa wenyeji. Fainali itafanyika  Jumamosi, Juni 8, mwaka huu.

Loading...

Toa comment