The House of Favourite Newspapers

Sanchez Azindua Sanamu Yake Chile Tocopilla, Chile

Na Mwandishi Wetu/ CHAMPIONI/GPL

HESHIMA aliyonayo Alexis Sanchez nchini kwao Chile ni ya kipekee, licha ya kuwa nchi hiyo imejaza mastaa kadhaa akiwemo Arturo Vidal. Ishu ni kwamba mshambuliaji huyo wa Arsenal, juzi alizindua sanamu yake aliyotengenezewa nchini humo.


Staa huyo raia wa Chile, imekuwa ikielezwa kuwa anaweza kuondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu huu, juzi alitua kwenye mji aliozaliwa wa Tocopilla ambako alikwenda kuzindua sanamu yake.
Watu wengi walijazana kwenye mji huo wakati wakimuangalia mchezaji huyo akikata utepe pamoja na kwamba walitoka Argentina ambako walilala kwa bao 1-0 na timu ya taifa ya nchi hiyo katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia na kuwa kwenye hali ngumu ya kufuzu.
Chile kwa sasa wapo katika nafasi ya sita kwenye Ukanda wa Amerika ya Kusini kwenye nchi zinazotafuta nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia, inatakiwa imalize ndani ya tano bora ili ipate matumaini.

Comments are closed.