The House of Favourite Newspapers

Sanchez: Mbwa Wananipa Mafanikio

0

MOSCOW,URUSI

STAA wa Arsenal, Alexies Sanchez ni kati ya wache­zaji mahiri sana kwenye soka akiwa na uwezo wa hali ya juu kutokana na kiwango chake ambacho amekuwa akikionyesha uwanjani.

Sanchez raia wa Chile ame­kuwa bora kwenye misimu kadhaa iliyopita na sasa yupo na timu yake ya taifa ya Chile kwenye michuano ya Kombe la Mabara nchini Urusi.

Staa huyo juzi alicheza mch­ezo wake wa kwanza kwenye michuano hiyo wakati timu yake ya Chile ilipovaana na Cameroon na kufanikiwa kushinda kwa mabao 2-0.

 

Sanchez, ambaye alianzia nje kwenye mchezo huo na ku­ingia kipindi cha pili ndiye ali­yechangia ushindi wa timu hiyo kwani wakati anaingia uwan­jani timu hizo zilikuwa suluhu.

Kuingia kwa mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita aliifungia klabu yake ya Ar­senal mabao 24 kwenye Ligi Kuu England kuliwaamsha mashabiki wa Chile waliokuwa jukwaani na kuamini kuwa anaweza kuisaidia timu hiyo.

Sanchez alifanikiwa ku­toa pasi zote mbili za mabao kwenye mchezo huo na kumal­iza kiu ya mashabiki wa nchi hiyo, lakini ajabu ni kwamba baada tu ya kumalizika kwa mechi hiyo, alisema amekuwa akipata mafanikio kwenye soka kwa kuwa anamiliki mbwa wawili.

Sanchez amesema mbwa hao ndiyo wamekuwa msaada mkubwa kwake na ndiyo ma­rafiki wake wakubwa.

 

Amesema mbwa hao ambao wanajulikana kwa jina la Atom na Humber, wamemsaidia kwa mafanikio aliyoyapata kwenye kikosi cha Arsenal na kwa mi­aka mingi kwenye timu ya taifa.

Mbwa hao ni maarufu sana kwa mashabiki wa Arsenal am­bao wamekuwa karibu kwenye kila mchezo wanabandika ban­go la kuwaonyesha kwenye Uwanja wa Emirates.

“Mimi ni mchezaji wa ki­mataifa na kila kitu ninachoki­fanya lazima kiwe cha kisasa zaidi, sipendi kwenda nje na siwezi kula nje ya nyumbani kwangu.

“Nimekuwa ni­kibaki nyumbani na mbwa wangu, wamekuwa wakini­saidia sana kupumzi­ka na kufanya kila kitu kwa ufasaha.

“Nimekuwa nikiongea nao na tumekuwa tukitoka wote kutembea nje, hali hii imekuwa ikinisaidia sana ku­fanya vizuri kwenye soka.

 

“Kwa sasa sifurahii maisha hapa kwenye michuano hii kwa kuwa nipo nao mbali la­kini nikikumbuka msaada wao natamani kufanya vizuri kwa kuwa nafahamu kuwa wana­taka nipate mafanikio,” alisema mshambuliaji huyo mahiri.

Sanchez ambaye anamali­za mkataba wake na Arsenal mwishoni mwa msimu ujao ni kati ya wachezaji ambao wa­nawindwa sana kwenye usajili barani Ulaya kwa sasa.

Mshambuliaji huyo anawindwa na timu kadhaa kubwa, Bayern Munich, Juven­tus, Manchester City na Chel­sea na kumekuwa na hofu kubwa kuwa anaweza kuondoka kwenye timu hiyo.

“Kwangu michuano hii ni muhimu sana, nafikiri natakiwa kuonyesha uwezo wangu na kuhamasishana kama timu ili tuweze kupata mafanikio hapa.

“Kumbuka tulifanikiwa kut­waa ubingwa wa FA tukiwa na Arsenal na hivyo tayari msimu huu nina kombe moja, yat­akuwa mafanikio makubwa sana kwangu kama nitatwaa na ubingwa huu.

“Sioni kama ni muda sahihi wa kuzungumza kuhusu suala la kujiunga na timu gani bado nina mkata­ba na Arsenal nafikiri hilo ndiyo jambo la msingi kwangu,” alise­ma Sanchez.

Staa huyu ambaye amefani­kiwa kuzichezea timu sita hadi sasa, zikiwemo kubwa za Bar­celona, Udinese na Arsenal amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 523 na kufunga mabao 163, tayari ameshaichezea timu yake ya taifa ya Chile michezo 108 na kufunga mabao 37.

Leave A Reply