The House of Favourite Newspapers

Sanchi Afungukia ‘Sanchi Feki’ Kuuzwa Dubai

Jane Rimoy ‘Sanchi’

KWA wafua­tiliaji wa mitandao ya kijamii wa­takuwa wameona ile habari iliyotrendi sana inayomhusu staa aliyefungashia Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ ya kwamba alipata dili la kwen­da kuhosti shoo huko Dudai huku pia akiongezewa dau kwa ajili ya kwenda kutoa penzi kwa ki­gogo mmoja wa huko.

 

Kama ni hivyo, basi habari iku­fikie kwamba, mchongo ule ulikuwa ni feki na inaonekana kuna mtu kulicheza dili hilo kwa nia ya kutapeli ama kumcha­fulia jina Sanchi.

Akiizungumzia skendo hiyo iliyowashangaza wengi, Sanchi alisema kuwa, yeye siye aliyehusika kwenye mawa­siliano hayo bali anaamimi kuna watu wamefanya ili kumchafulia jina lake.

 

“Najua wazi kabisa kuna watu hawapendi maendeleo ya watu wengine hivyo wanatafuta kila namna kuwachafua kwa sababu najua wazi ni vitu vya kutengeneza na ndio maana sijahangaika nao kabisa, naona wanajihangaisha tu.

“Kama kuna Sanchi alitakiwa kwenda Dubai kuhosti shoo na kulala na pedeshee, huyo atakuwa Sanchi feki,” alisema Sanchi.

STORI: IMELDA MTEMA, IJUMAA

 

MOBETO: NYUMBA TUNAYOISHI IMETOKA KWA DIAMOND – VIDEO

Comments are closed.