The House of Favourite Newspapers

SANCHI AJIANDAA KUMPA MAMA’KE MJUKUU

Jane Rimoy ‘Sanchi’

M WANAMITINDO mwenye figa matata Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ amesema kuwa yuko mbioni kumpa zawadi ya mjukuu mama yake mzazi, kwani anaamini zawadi hiyo itakuwa nzuri sana kwa mama yake huyo na hata kwake pia.

Akizungumza na gazeti hili, Sanch alisema kuwa mama yake amekuwa na hofu kutokana na kazi yake ya uanamitindo na kuzunguka nchi mbalimbali kwamba itakuwa ngumu kwake kuweza kutulia na kubeba ujauzito mpaka kujifungua.

“Kwa kweli niko mbioni kumpa mama yangu zawadi ya mjukuu maana amekuwa na wasiwasi sana kutokana na kazi yangu ninayofanya anaona labda nitachelewa sana kumpatia mjukuu hivyo nataka kwenye hilo nisimuangushe nalifanyia kazi,” alisema Sanch bila kuainisha atazaa na nani.

STORI: Imelda Mtema

Comments are closed.