Sanchi Atoa Ushauri kwa Wanaume ‘Acheni Kutangatanga’

Modo maarufu nchini Tanzania na mrembo anayefahamika sana kwenye mitandao ya kijamii, Jane Rimoy almaarufu kama Sanchi ametuma ujumbe mzito kwa wanaume kuhusu suala la uaminifu katika ndoa. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Sanchi amewataka wanaume kuwa na msimamo wa kweli katika mapenzi kwa wake zao badala ya kutangatanga nje ya ndoa.
Katika ujumbe wake, Sanchi alisema:
“Wanaume wanapaswa kukomaa kuwapenda wake zao kuliko kutoka nje ya ndoa. Komaa na mkeo wewe, wazuri hawaishi.” 😊
Kauli hiyo imezua mijadala mitandaoni, ambapo baadhi ya wafuasi wake wameunga mkono wakisema ni ushauri wa hekima, huku wengine wakichukua fursa hiyo kuzungumzia changamoto katika ndoa za kisasa.